Mshambuliaji mpya wa PSG, Neymar hataweza kushuka uwanjani kuichezea timu yake hiyo leo kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya masuala ya nyaraka za uhamisho wake.
Neymar ambaye alitua jana katika kikosi hicho cha Paris Saint-Germain alisema yupo tayari kucheza katika mchezo wa leo dhidi ya Amiens.
Inaelezwa kuwa kuna documents kuhusu risiti za uhamisho wa kimataifa ambazo zinatakiwa zipatikane ili aweze kuanza kufanya kazi.
Lakini mamlaka za soka za Ufaransa zimechelewa kupata nyaraka hizo kutoka Hispania.
0 comments :
Post a Comment