News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday, 1 August 2017

MWINYI HAJI NGWALI: HIO SOUTH AFRICA YAO KAMA MOROGORO TU AU TATIZO JINA ?


Morogoro. WAKATI Simba, wakitambia uwepo wao Afrika Kusini, beki wa Yanga, Haji Mwinyi hajaumizwa na hilo kwa madai sehemu walikojichimbia hapa Morogoro ni kama Sauzi tu.
"Afrika Kusini kwa sasa kuna baridi kali,huku Morogoro tupo maeneo ya Mlimani ambapo baridi lake ni kali mno, uwanja ni mzuri ambao unatufanya tuwe na maandalizi ya aina yake, ndiyo maana nimesema Sauzi ni kama Morogoro tu,"alisema
Alielezea kwamba kinachotakiwa ni kujiandaa vya kutosha na siyo umarufu wa sehemu kwa madai  matunda ya kambi hizo yataonekana uwanjani na siyo maneno ya mitaani.
"Mwisho wa yote zote ni kambi tu, ila cha kuzingatia katika kambi hizo kinafanyika kitu gani cha kufanya timu iwe na maendeleo yanayotakiwa,mfano sisi baridi la huku linatufanya tufanye mazoezi kwa muda mrefu bila kuchoka,"alisema
Alitolea mfano pindi Simba, ilipokuwa chini ya  Dylan Kerr,ambaye kwa sasa anaifundisha Gor Mahia ya Kenya, kwamba waliweka kambi Lushoto ambako kuna baridi ambalo liliwasaidia kujijenga zaidi.
Alizungumzia kuhusiana na ushindani unaoendelea kwenye mazoezi kwa ajili ya kumshawishi kocha Mzambia George Lwandamina, anayechunguza kikosi cha kwanza kwamba ni mkali kila mchezaji anaonyesha juhudi zake.
"Unapokaribisha wageni haina maana kwamba uliyekuwepo na timu ulale na kujibweteka, ikumbukwe kwamba soka ni kazi inayomfanya kila mtu aendeshe maisha yake, hivyo lazima kujituma na mwisho wa yote itajulikana nani alikuwa makini kwenye mechi,"alisema.
CREDIT:  mwanaspoti
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment