News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 5 August 2017

MANJI ARUDISHWA RUMANDE RUFAA YAKE YAGONGA MWAMBA


Ombi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji la kutaka apewe dhamana katika kesi inayomkabili ya uhujumu uchumi, limeendelea kuwa gumu baada ya
leo Ijumaa kushindwa kutolewa uamuzi kutokana na Jaji Isaya Arufani wa Mahakama Kuu ya Tanzania kutokuwepo mahakamani hapo kusikiliza ombi hilo.
Manji alipeleka maombi hayo katika mahakama hiyo kupinga hati iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuzuia dhamana dhidi yake.
Kutokana na jaji huyo kutokuwepo, ombi hilo limesogezwa mbele na linatarajiwa kusikilizwa Agosti 7, mwaka huu.
Kumbukumbu zinaonyesha Manji ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Yanga na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali jambo ambalo ni kinyume cha sheria. 
Katika kesi hiyo ambayo inaendeshwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Huruma Shaidi, leo asubuhi ilitajwa katika mahakama hiyo na kuahirishwa hadi Agosti 9, mwaka huu kutokana na Manji kutofika mahakamani hapo.
Manji alishindwa kufika mahakamani Kisutu kutokana na kuwa na kesi katika Mahakama Kuu.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment