News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 30 August 2017

MAKALA DOMO KAYA:KUNA HAJA YA KUWAULIZA WACHEZAJI MASELA NGOTO WANAVYOJISIKIA KWA SASA


ABDI Hassan Banda kafunga bao lake la kwanza akiwa na jezi ya Baroka. Ilikuwa ni katika pambano dhidi Orlando Pirates.
Nilitazama mechi yote na Banda alinikosha sana. Orlando Pirates hawakujua uhodari wake wa kucheza mipira ya juu.
Aliruka hewani na kupiga kichwa cha nguvu kilichomshinda kipa wa Orlando Pirates. Lilikuwa bao la kusawazisha. Baadaye aliibusu nembo ya timu yake mpya na kuzungukwa na wachezaji wenzake waliokuwa ndani na wale waliokuwa katika benchi. Unapata hisia gani nzuri zaidi ya ukiwa mchezaji wa kulipwa katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini?.
Simon Msuva hakamatiki kwa sasa kule kwa Waarabu wa Morocco. Juzi alifunga bao la nne wakati wakicheza mechi ya Kombe la Ligi nchini huo. Tangu afike amekuwa nyota katika klabu yake. Amekuwa anazichezea nyavu.
Kwa harakaharaka, hawa wawili wameungana na Mbwana Samatta, Farid Mussa na Thomas Ulimwengu ambao walitangulia. Ulimwengu anasumbuliwa na goti lakini Samatta tayari ashaizoea Ulaya na Ulaya imeshamzoea. Anafunga kadiri anavyojisikia.
Kila siku tunapita mitandaoni na kusikia habari zao. Dunia imekaa katika kiganja na ni rahisi kusikia wanachosema wakielezea furaha zao kucheza nje ya mipaka yetu. Pengine wanatoa somo kubwa kwa vijana wanaotaka kucheza Ulaya.
Hata hivyo, hawa waliokwenda nje ya mipaka yetu ni wachache kuliko wachezaji wetu masela fulani hivi ambao wamepita katika kizazi hiki cha katikati. Wapo waliokuwa na vipaji vikubwa kuliko kina Banda na Msuva ambao walau wamejaribu.
Tulipitia kizazi kipya cha miaka ya karibuni ambapo baadhi ya wachezaji wetu walikuwa wanapiga soka maridhawa sana, lakini kila siku malalamiko juu yao ikawa ni suala la nidhamu. Wengi kati yao wamepotea. Maisha yanaanza kuwapiga taratibu.
Hawa nao inabidi wafuatwe kwa akili na waulizwe kuhusu majuto yao. Inawezekana pia majuto yao yakawatia moyo maelfu ya vijana wanaotamani kuwafikia kina Samatta. Inawezekana majuto yao pia yakawa chachu kwa vijana wanaoibuka kwa sasa.
Katika maisha kuna stori za aina mbili. Kuna hizi za mafanikio na kuna zile za majuto, hasa kama mwanadamu anajuta mwenyewe kwa kupoteza fursa zilizojitokeza. Nawafahamu wanasoka kadhaa ndani ya miaka 10 hii ambao wanajuta kisirisiri lakini hawataki kusema wanajuta.
Wanasoka hawa wanajua wangeweza kwenda mbali zaidi ya Samatta au wangeweza kujaribu kama akina Banda. Mungu ndiye anayeamua lakini mwanadamu analazimika kujuta. Kila siku tulikuwa tunawaambia wanasoka hawa waachane na mambo ya bangi na sifa za Uwanja wa Taifa wajikite katika maisha yao ya siku za usoni.
Wengi walihisi tunawaonea wivu. Leo inawezekana wana majuto ambayo wanaweza kutuambia. Klabu zao za sifa, Simba na Yanga zimewatupa na hata mashabiki nao wamewatupa kwa sababu mashabiki na timu zetu huwa wananyanyuka na mtu ambaye anaibeba timu kwa nyakati hizo.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment