KUDADADEKIII!! CHUPA YA MAJI YALETA BALAA GOLINI JAMAA WALIKUA WANAKOSA MAGOLI WAO NA MSTARI ILIVYOTOLEWA MPIRA MMOJA TU KAMBAAA!!
Serengeti. Mashabiki wa Kibeyo FC juzi walizua jambo baada ya kuamua kuvamia lango la timu ya Muungano na kuchukua chupa ya maji iliyokuwepo langoni hapo kwa madai ndio iliyokuwa ikifanya wakose
mabao ya wazi.
Mchezo huo ulikuwa wa Ligi ya Mapesa Cup ambao ulipigwa katika uwanja wa Sokoine mjini hapa.
Katika mtanange huo, Muungano walikuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao ambapo bao hilo lilifungwa na Yohana Nyakonga dakika ya
37.
Baada ya bao hilo, Kibeyo walianza kufanya mashambulizi ya nguvu langoni mwa wapinzani wao ambapo wachezaji wa timu hiyo walikosa mabao
ya wazi.
Hatua ya kukosa mabao ya wazi yaliwashtua mashabiki na wachezaji wa timu hiyo ambapo waligundua kuwa chupa iliyokuwa langoni mwa wapinzani
wao ndio iliyosababisha hali hiyo.
Mashabiki hao na wachezaji wa timu hiyo dakika ya 80 waliamua kuvamia lango la wapinzani wao na kwenda langoni mwa wapinzani wao kutaka kuchukua chupa hiyo.
Hata hivyo mwamuzi wa mchezo huo Changala Mauma aliepusha shari na kuamua kuitoa chupa hiyo na mchezo kuendelea.
Baada ya kuitoa chupa ile dakika ya 82 Kibeyo waliweza kusawazisha bao hilo ambalo lilifungwa na Straika Karaki Kisuka.
Bao hilo liliamsha shangwe kwa mashabiki hao huku wakidai bila ya kutoa ile chupa langoni wazingeweza kusawazisha.
0 comments :
Post a Comment