News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 27 August 2017

HEBU SOMA DHARAU ZA KIPA WA YANGA KWA WAZEE WA WIKI aka 7G SIMBA KABLA YA KUANZA PAMBANO LAO DHIDI YA LIPULI


KIPA namba moja wa Yanga ambaye juzi alifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo ya Simba, Youthe Rostand raia wa Cameroon amesema kuwa wapinzani wao ni wa kawaida sana tofauti na ilivyokuwa ikielezwa kwenye vyombo vya habari. Kipa huyo ambaye alipangua penalti ya Shabalala amesema
kuwa haoni kama Simba inaweza kuwa kikwazo kwao kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo jana iliibanjua  Ruvu Shooting 7G au 7-0  “Ule ulikua ni mchezo wangu wa kwanza mkubwa tangu nifike hapa nchini lakini kwa jinsi nilivyoitazama Simba sioni kwamba ni timu inayoweza kuwa kikwazo kwetu kutetea taji,” amesema kipa huyo. “Unaweza kuona namna tulivyowadhibiti kuanza mwanzo wa mchezo hadi dakika ya mwisho, suala la penalti linajulikana kwasababu katika hatua hiyo jambo lolote linaweza kutokea uwanjani,” aliongeza. Kiwango cha kipa huyo katika mchezo huo pia kilikuwa gumzo kwa mashabiki ambao tayari wameonekana kuanza kumsahau Dida aliyetimkia Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment