Muda mfupi baada ya Simba kuifunga Yanga kwa penati, Jumatani ya wiki hii katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, utani wa jadi baina ya timu hizo umeendelea.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametumia ukurasa wake wa Instagrama kumtania mshambuliaji wa Yanga Ibrahimu Ajibu kwa kumshauri arejee Simba kwa kuwa Yanga kuna njaa.
Haji Manara ameyaandika haya:
“Ahhh mwana,umepishana na fuko la Money!! huko Swaumu huku MO Money nimebonyezwa miezi miwili no Salary, ukiona vp rudi tu,,huku home bana 😂😂😂 @ibrahimajibu23 @shaffih”
Kabla ya hapo aliweka takwimu za mchezo huo kisha kuandika hivi: Ipo mijitu lazma ikapimwe mkojo,,eti inashangilia kufungwa,mara Shimbimbi mara Shilole!!khamsa mmelamba na kwa takwimu tumewazidi! Shubamit 😊😊”
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment