Kiungo mpya wa Simba, Nicholas Gyan anatarajia kutua nchini ndani ya siku mbili akitokea kwa Ghana.
Gyan alikwenda kumaliza majukumu kadhaa kama alivyokuwa amekubaliana na Simba na anatarajia kutua nchini kuanza kazi.
Mmoja wa viongozi wa Simba amesema: "Mimi si msemaji lakini Gyan anakuja ndani ya siku mbili. Mashabiki na wanachama waondoe hofu.
"Tumesikia watu wakisema alikuja kama shoo na kuondoka. Lakini Gyan ni mcheaji wetu na anakuja."
Gyan alionyesha kiwango safi katika mechi ya kirafiki wakati Simba ilipocheza na Rayon Sports wakati wa Tamasha la Simba Day.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment