News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 20 August 2017

BI HINDU AMGEUKA MZEE KILOMONI, ALEGEZA MSIMAMO KUHUSU MABADILIKO YA SIMBA



Licha ya kuwa mzee Hamisi Kilomoni bado anashikilia msimamo wake wa kutokubali mabadiliko ya kimfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba, mzee mwenzake Chuma Suleiman maarufu kwa jina la Bi Hindu ameanza kulegeza msimamo.
Bi Hindu ambaye alikuwa pamoja na mzee Kilomoni katika kupinga mabadiliko hayo ya kimfumo, ameonyesha wazi kuwa sasa ameanza kulegeza msimamo wake kwa kusema kuwa yeye anachowaza kwa sasa ni timu hiyo kuifunga Yanga.
Kuhusu mabadiliko hajui chochote kwa kuwa hakwenda kwenye mkutano wa wanachama uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar na kama wameamua hivyo kwake sawa tu lakini hana cha kusema zaidi.


* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment