News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 27 August 2017

ARSENAL YACHAPIKA 4-0 aka "4G" WATOTO WA MJINI WANAITA MIGUU YA MEZA


Mara ya mwisho Arsenal  kushinda katika uwanja wa Anfield ilikuwa mwaka 2012, hii leo washika mitutu hao wa London wameendeleza rekodi mbovu Anfield baada ya kupigwa kipigo cha bao 4 kwa 0.
Alianza Roberto Firminho dakika ya 17 kabla ya Sadio Mane kufunga dakika ya 40 na kuwa mchezaji wa pili kuifungia Liverpool mabao katika mfululizo wa mechi tatu za mwanzo wa msimu, mabao hayo yalikifanya kipindi cha kwanza Liva kwenda mapumziko wakiongoza kwa mabao mawili Kipindi cha pili Mohamed Salah ambaye ndio mchezaji bora wa mchezo huu alifunga la tatu dakika ya 57 kabla ya Daniel Sturidge dakika ya 77 likiwa ni goli lake la 99 kwa Liverpool na kuufanya mchezo uishe kwa matokeo ya 4 kwa 0.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment