KLABU ya Yanga inatarajia kuwahisha usajili wa wachezaji wapya mapema kabla ya Mfumo wa Mtandao wa Kimataifa (TMS) kufungwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Msimu uliopita Yanga walipigwa faini Sh milioni tatu baada ya kuchelewesha usajili wa wachezaji, jambo ambalo viongozi wa klabu hiyo hawataki litokee msimu huu.
Akizungumza na MWANASPORTS LEO BLOG, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema wamepanga kukamilisha usajili kabla ya dirisha kufungwa Agosti 6, mwaka huu.
Mkwasa alisema malengo yao ni kuwasilisha mapema usajili kabla ya klabu nyingine, wakiwamo wapinzani wakuu wa soka Simba.
Alisema watawatambulisha wachezaji wapya muda wowote kuanzia sasa.
Mkwasa alisema kwa kuwa wanajua mahitaji yao, hakuna haja ya kukaa muda mrefu na kusubiri dakika za mwisho za dirisha kufungwa ili kuepuka usumbufu unaojitokeza mara nyingi.
“Kipindi hiki hatutasubiri siku ya kufunga dirisha, mapema tu tutamaliza usajili wetu na kila Mwanayanga atajua kikosi chao kwa sababu tutawatambulisha wachezaji wote tuliowasajili, ambapo kwa sasa zimebaki nafasi chache kulingana na ripoti ya mwalimu,” alisema Mkwasa.
Mkwasa alisema kamati ya usajili waliyoiteua inafanya kazi yake kwa umakini na wanaamini watapata wachezaji wenye uwezo wa kukitumikia kikosi chao
![](https://is05.ezphotoshare.com/2017/07/17/snRRYI.jpg)
![](https://is02.ezphotoshare.com/2017/07/23/sAYGYx.jpg)
0 comments :
Post a Comment