News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday 28 July 2017

NI KITU GANI KIMEMPATA NGOMA MPAKA AITOLEE CLUB YAKE KAULI HII??


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe amesema kuwa anahisi ana deni ndani ya moyo wake ambalo anapaswa kulilipa baada ya kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu bara na ile ya Klabu Bingwa Afrika ambayo watashiriki. Ngoma amesema kuwa viongozi wa klabu ya Yanga wamekuwa waungwana kwake katika kipindi chote ambacho alikuwa nje ya kikosi akiuguza majeraha ya goti na kuhusishwa kutaka kutua kwenye kikosi cha Simba. “Nipo fiti kimchezo baada ya kupona kabisa jeraha langu la goti, nadhani ni muda wangu wa kulipa fadhila kwa viongozi baada ya kunivumilia kwa kipindi kirefu,” alisema Ngoma. “Yanga ni sehemu tofauti kabisa kwa sababu pamoja na kukaa nje ya kikosi kwa muda mrefu lakini nimepokelewa kwa mikono yote miwili sambamba na kupewa mkataba, klabu imeonyesha nia ya kuendelea na mimi katika mazingira yote hivyo napaswa kulipa fadhila Ligi zitakapoanza,” aliongeza Ngoma. 
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment