Mshambuliaji mpya, Alvaro Morata aliyesajiliwa Chelsea kwa dau la Pauni Milioni 70 kutoka Real Madrid wiki iliyopita akipasua katikati ya wachezaji wa Bayern Munich katika mchezo wa Kombe la Mabingwa wa Kimataifa leo Uwanja wa Taifa mjini Singapore. Bayern Munich imeshinda 3-2 mabao yake yakifungwa na Rafinha dakika ya sita na Thomas Muller mawili dakika ya 11 na 26, wakati ya Chelsea yamefungwa na Marcos Alonso dakika ya 45 na ushei na Michy Batshuayi dakika ya 86
0 comments :
Post a Comment