Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin ameelezea ushindani unaoendelea katika kambi waliyoweka mkoani Morogoro kwamba, unaonyesha taswira wa jinsi ambavyo kikosi cha kwanza cha timu hiyo kitakavyokuwa moto wa kuotea mbali.
"Maandalizi ya msimu yanamfanya mchezaji ajitume kwani unakuwa ni wakati wa kocha kuchagua kikosi chake cha kwanza, hivyo mazoezi na ushindani yaliyopo baina yetu si mchezo," anasema.
Martin alisema ushindani unaoendelea unasaidia kupandisha viwango vyao kwani kila mmoja anataka kuonekana mbele ya kocha Mzambia Goerge Lwandamina ili aweze kupata namba katika kikosi cha kwanza.
"Nimeamini mchezaji akitumia vyema maandalizi ya msimu anakuwa mzuri wakati ligi ikiendelea kwani mazoezi tunayoyafanya ni ya kufa mtu," alisema.
0 comments :
Post a Comment