News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday 15 July 2017

MCHEZAJI AJAX ALIEITWA DOGO FUNDI ADONDOKA UWANJANI NA KUPOOZA KABISA MADAKTARI WASEMA HAWEZI TENA....



Timu ya Soka ya AJAX imethibitisha kwamba  Mchezaji wake kinda Abdelhak Nouri "Appie" aliyeanguka uwanjani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Weder Bremen amepata Matatizo ya Kudumu katika Ubongo na nafasi ya kupona na kurejea uwanjani ni "Nill" (0).

Nouri mwenye Miaka 20 na kipaji cha hali ya juu amekuwa akitarajiwa kuwa Nyota wa Uholanzi kwa siku za Usoni lakini inavyoonekana ndoto za Kijana huyu,Ajax na Uholanzi zimefika Ukomo, its terrible, ni Mungu pekee awezae kumponya,

Vipimo vya MRI kwenye Ubongo vinaonyesha kwamba ubongo wake haufanyi kazi kwa kukosekana kwa Oxygen Supply, na kabla ya kuanguka uwanjani katika dk ya 70 alipata mashambulio kadhaa ya Moyo, baada ya kupata matibabu ya awali amerejeshwa Uholanzi, kwa sasa hawezi kuongea,kula, kutembea wala kufanya chochote, Madaktari wanasema  hatopona.

Ashindwacho Binadamu Mungu hashindwi, Mungu na akasimame katikati yake na Familia yake kuwapa Tumaini na hata kumponya: Amen.

Pio Pius...😭😭😭
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment