News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday 8 July 2017

Maswahiba wanaokwenda kuwa Wachezaji ghali Uingereza wakijifua pamoja



Wakiwa wanaelekea kuwa wachezaji 'pacha' ghali zaidi katika Premier League - Romelu Lukaku na Paul Pogba wanajifua vilivyo kwenye likizo yao huko Marekani. Jose Mourinho anaamini kuwa klabu yake imefikia makubaliano na Everton ya kumnunua Lukaku kwa pauni milioni 75 ambayo itamfanya awe mchezaji ghali wa pili katika Premier League nyuma ya Paul Pogba aliyenunuliwa kwa pauni milioni 89. Wawili hao wenye urafiki wa hali ya juu, wako mapumzikoni Los Angeles na wamekuwa wakijifua pamoja tayari kwa msimu mpya. Lukaku anategemewa kufanya vipimo vya afya huko huko Los Angeles na inaaminika kuwa dili hilo lina ushawishi mkubwa kutoka kwa Pogba. 
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment