News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday 6 July 2017

MADIWANI 19 WA CUF WAUNGANA NA HALIMA MDEE WAPINGA KUKAMATWA KWAKE WASEMA....

Madiwani 19 wa CUF wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam wamelaani agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi la kuagiza Polisi kumkamata na kumuweka ndani, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAVICHA) na Mbunge wa Kawe Halima Mdee, kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi wakati alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu agizo la wanafunzi wanaopata ujauzito kutorudi shule.
Akizungumza kwa niaba ya madiwani hao, Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mussa Kafana,amesema agizo hilo limekiuka sheria za nchi, kwa kuwa Mdee alitumia haki yake kikatiba kujieleza na kutoa maoni yake kuhusu agizo la Rais John Magufuli la kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kurudi shuleni baada ya kujifungua.
“Halima anao uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake, alichofanya mdee sio kosa, ni mjumbe wa Baraza la Halmashauri ya jiji, na la Kinondoni. Ikumbukwe kwamba kila anayetoa maoni yanayopingana na serikali siyo mhasi na ahatakiwi kuchukuliwa hatua,” amesema Kafana.  
Mnamo Julai 3, 2017 jijini Dar es Salaam, Mdee wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuwa agizo la wanafunzi wanaopata ujauzito kutorudi shule baada ya kujifungua ni kinyume na sheria ya mtoto ya mwaka 2009, huku akizitaka halmashauri zinazoongozwa na Chadema kuruhusu watoto hao kurudi shule. 
Na Regina Mkonde
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment