News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday 27 July 2017

DEAL DONE:TSHISHIMBI ASAINI MIAKA MIWILI YANGA,JUMAPILI KIFAA KINGINE KIPYA KUTANGAZWA


,Dar Es Salaam.

MABINGWA wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara,Yanga SC jioni ya leo wametangaza kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Kongo,Papy Kabamba Tshishimbi aliyekuwa akiichezea Mbambane Swallows ya Swaziland.

Hilo limewekwa wazi usiku huu na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo,Hassan Nyika wakati akifanya mahojiano na kituo cha Redio cha EFM na kuongezea kuwa kiungo huyo aliyetua nchini tangu wiki iliyopita amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya taratibu zote kukamilika ikiwemo kufanyiwa vipimo vya afya.
Tokeo la picha la tshishimbi of mbabane swallows

Wakati huohuo Nyika amewataka mashabiki na wanachama wa Yanga wakae mkao wa kula kwani siku ya Jumapili watatangaza nyota mwingine mpya waliyemsajili.

Habari za ndani zinasema nyota huyo mpya huenda akawa kiungo wa Mbeya City,Raphael Daudi ambaye ametajwa kuingia kandarasi ya miaka miwili.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment