Baadaya kumnasa Ditram Nchimbi kutoka Mbeya City ili kuimarisha safu yake ya ushambulizi, Lipuli ya Iringa imemnasa Malimi Busungu.
Busungu amejiunga na Lipuli kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mshambuliaji huyo alikuwa hatari wakati akiwa Mgambo FC ya Tanga hadi alipojiunga Yanga.
Msimu wa kwanza akiwa Yanga alionyesha cheche lakini kuanzia katikati mambo yalibadilika mwisho akapotea mwelekeo.
Hata hivyo, Busungu niliwahi kufanya nae mahojiano tukiwa wote mzumbe na aliniambia angependa kuondoka Yanga na kwenda kuanza upya na anajiamini atafanya vema.
0 comments :
Post a Comment