News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday 13 July 2017

Aveva, Kaburu warudishwa mahakamani

aveva
Dar es Salaam. Wakati akili, masikio na macho ya mashabiki wa soka nchini leo Alhamisi  yakielekea Uwanja wa Taifa kuishuhudia Everton ya Wayne Rooney ikicheza na Gor Mahia ya Kenya, Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' watapandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za klabu pamoja na kutakatisha pesa ambapo wapo rumande tangu Juni 29 kutokana na tuhuma hizo kukosa dhamana.
Vigogo hao wawili walifikishwa mahakamani hapo baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuona wana mashitaka ya kujibu.
Tuhuma hizo zinahusisha kutakatisha kiasi cha dola 300,000 (zaidi ya Sh 650 milioni).
Watuhumiwa hao walisomewa mashitaka matano na mawakili wa serikali chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa lakini haikuweza kusikilizwa kutokana na uchunguzi kutokamilika.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment