News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday 17 July 2017

ASHAANZA KIBURI: SIMBA LETENI MILIONI 60 NISAINI HAMTAKI NAENDA.....


KIPA bora wa michuano ya Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), Said Mohamed ‘Nduda’, amesema yuko tayari kujiunga na timu yoyote ambayo itakuwa tayari kumpa kitita cha Sh milioni 60.
Nduda kwa sasa yuko huru baada ya mkataba wake na klabu aliyokuwa akiitumikia ya Mtibwa Sugar kumalizika msimu uliopita.
“Mimi dau langu ni Sh milioni 60, timu itakayonipa hizo fedha niko tayari kuichezea,” alisema Nduda.
Kuhusu uwezekano wa kujiunga na Simba ambayo imehusishwa kumwania alisema;
“Tupo kwenye mazungumzo kama watakuwa tayari kutekeleza masharti yangu nitasaini, ila kwa sasa sijaridhika na dau lao,” alisema
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment