News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday 24 June 2017

KOTEI AWALETEA SIMBA SC MBADALA WA IBRAHIM AJIB A+A- Soma zaidi hapa



UKISUSA wenzio wanakula! Hivyo ndivyo mambo yanavyozidi kunoga ndani ya kikosi cha Simba ambapo mchezaji kiraka wa wekundu hao, James Kotei alipopata taarifa ya kuondoka kwa Ibrahim Ajib akatingisha kichwa. Kisha ameuambia uongozi wake kuwa anatarajia kutua wakati wowote nchini huku akiambatana na bonge la straika ambaye ana kazi moja tu ya kupachika mabao. Taarifa ambayo   Mwana sports leo blog "mama ya blog hii"  inazo, ni kwamba Kotei ameshapata baraka za kumleta straika huyo ambaye ana uwezo wa kucheza katika namba zote za idara ya kiungo na ushambuliaji. Tayari saluti5 inatambua pia jina la kifaa hicho na klabu anayotoka, lakini uongozi wa wekundu wa Msimbazi umeweka sharti la kutoweka bayana kila kitu kwa sasa kwa sababu ya kuepuka figisu za masuala ya usajili. “Wakati wowote Kotei atatua kwa ajili ya kujiandaa na kambi ya mazoezi ya Ligi Kuu na bonanza la Simba Day lakini anakuja na straika kama mrithi wa Ibrahim Ajib, kwasababu ana uwezo wa kumiliki mpira na kucheza zaidi ya namba nne katika idara ya kiungo na ushambuliaji.” “Ni kama alivyo mwenyewe Kotei ambaye ni mchezaji kiraka, ndivyo alivyo mchezaji huyo anayekuja nae anayetoka katika timu inayocheza Ligi Kuu ya nchini Ghana na yumo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Ghana,” kilieleza chanzo chetu makini ndani ya Sinba. Katika hatua nyingine, james Kotei ameiambia Mwana sports leo kwa njia ya mtandao wa baruapepe kuwa, marafiki na ndugu zake wa karibu wan chi ya Ghana wameonyesha kuvutiwa na mwenendo wa timu ya Simba kwa kufanya usajili wa maana na kwamba jezi za wekundu hao zimekuwa kivutio kikubwa kwa Waghana hao. “Jezi zangu zote za Simba nilizokuwa nazo huku Ghana zimeporwa na ndugu na marafiki zangu, ninarudi sina hata jezi moja. Hii inanipa faraja kuwa hata wao wananiunga mkono kuitumikia Simba yangu hii,” alisema Kotei.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment