News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday 27 May 2017

YANGA BHANAAA!! SIKILIZA MAJIGAMBO YA VIONGOZI KUHUSIANA NA MAJINA YA WANAOKUJA YANGA MSIMU HUU

                                                          George Lwandamina Chicken


 

YANGA imesikia fujo zinazofanywa na Singida United kwenye usajili wa wachezaji tangu ilipopanda daraja na kurejea ligi kuu bara na pia imepata taarifa kuwa wapinzani wao wa Jadi,Simba tayari wameshamnasa nahodha wa zamani wa Azam FC,John Bocco Adebayor lakini Mjumbe wa wa kamati yake ya utendaji,Salum Mkemi amesema wao kama Yanga hawatishwi wala hawanyimwi kabisa usingizi na jambo hilo.

Akiongea kutoka Arusha alikoambatana na kikosi cha Yanga kilichowasili jijini humo jana Ijumaa kulitembeza kombe lao la ubingwa pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC,Mkemi amewataka mashabiki wa Yanga kutulia na kuacha uongozi ufanye kazi yake kwa maelekezo ya kocha wao Mzambia,George Lwandamina Chicken.

Amesema Yanga ni timu kubwa na inaweza kuchukua/kusajili mchezaji yoyote yule kutoka kokote kule.Wanachosubiri sasa wao kama viongozi,kocha aseme anamtaka nani wamletee kwani pesa ipo.

Wakati huohuo Mkemi amesema kesho Jumapili Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kucheza na AFC bila ya wachezani wake wanne ambao wako kwenye majukumu ya timu zao za taifa.

Mkemi amewataja wachezaji hao kuwa ni Hassan Ramadhani Kessy,Beno Kakolanya,Mwinyi Hadji Mgwali na Mnyarwanda Haruna Hakizimana Niyonzima.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment