News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday 30 May 2017

KWA HILI LAZIMA BARAKA DA PRINCE AMRUSHIE NGUMI MO MUSIC HUU NI UCHOKOZI WA NGUMI!!

Msanii wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’

MSANII wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’ ameonyesha kumchokonoa mwanamuziki mwenzake, Barakah The Prince baada ya kuibuka na kusema kwa kipindi kirefu amekuwa akimzimikia mwanadada Najma ‘Naj’ ambaye ni mwandani wa msanii huyo.

Akibonga na Mikito & Habari, Mo Music alisema kwa jinsi anavyomkubali mrembo Naj kama yeye ndiye angekuwa anatoka naye kimapenzi angeshamuoa kitambo kwani ni msichana mzuri na mwenye sifa za kuwa mke mwema hivyo akiona Barakah anazidi kumpotezea muda atatangaza ndoa haraka iwezekanavyo.

“Kipindi najipanga kumtokea Naj ndipo Barakah akaniwahi, lakini siku zinakatika anaishia kumuuzisha sura mitandaoni wakati mimi sikutaka kumpotezea muda kabisa, isitoshe wazazi wangu wamenisihi nioe mwaka huu kama itakaribia mwisho wa mwaka bado hajamuoa, mimi nitamchumbia Naj na kumuweka ndani,” alisema Mo Music.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment