Sababu kubwa aliyoitaja ni kwamba hadi sasa ameshatoa video mbili tu tangu arejee tena rasmi kwenye muziki hivyo haoni ulazima wa kuharakishia mambo. Moe amemuambia mtangazaji wa 24 RADIO kaka mkubwa GK kuwa anachofanya sasa ni kuijenga upya CV yake na pindi akitaka kumshirikisha mtu kuwepo na marejeo ya kutosha ya video zake mtandaoni.
“Huwezi kuwa na video moja, video mbili halafu uende labda kuomba kufanya collabo na msanii fulani wa nje ambaye mwenzako labda ana video kumi, kwahiyo lazima kwanza tutengeneze hiyo profile ikae vizuri,” amesema Jay Moe.
Rapper huyo amedai kuwa anapenda kuona siku moja pia wasanii wa nje nao wakiwaomba wasanii wa Tanzania collabo na hiyo itatokana na kuwepo kwa kazi nzuri zitakazowashawishi.
0 comments :
Post a Comment