News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 22 March 2017

AT adai Rama Dee amemkosea heshima Adam Juma


Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya msanii Rama Dee kusema kiwango cha ‘director’ Mkongwe Adam Juma kiko chini ya viwango katika kutayarisha na kutengeneza ‘video’ na kwamba anamtaka ajifunze kutoka kwa Hanscana kauli ambayo ilipigwa na wadau mbalimbali wa muziki.

“Imekuwa desturi kwenye nchi yetu mtu kutomuheshimu mwenzake au nguvu zake, leo unatoka unasema Adam Juma hajui ku-shoot ‘video’, wakati wewe ukipewa ile kamera hata kupiga picha huwezi kujua lakini yule mtu ndiyo amekuja muziki wa Tanzania”. AT alikiambia kipindi cha eNewz cha EATV
Aidha msanii huyo amesema wasanii ndiyo wanaongoza kwa kutokuwa na heshima, hivyo amewataka wasanii wenzake kuwa na heshima kwa watu waliowazidi.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment