
Akiongea kwenye kipindi cha cha redio moja nchini Jumapili, Nyauloso alidai kuwa producer wake ndiye aliyeongea na Vee kuhusu kushirikishwa kwenye ngoma yake.
Amedai kuwa badala yake Vee alionekana kutokuwa tayari licha ya Nyau kuamini kuwa anamfahamu vyema na waliwahi kushindania tuzo moja ya msanii anayechipukia.
Hata hivyo rapper huyo amedai kuwa yeye mwenye binafsi hajawahi kumuambia Vanessa kuhusu ombi lake la collabo. “Na nikukutana naye naona ananichekeaga tu,” alisema Nyauloso.
“Ni mtu ambaye anaonekana yuko happy, hana tatizo na mimi, sema ndio hivyo alikataa kufanya kwenye kazi yangu,” aliongeza.
Bongo5 imemtafuta Vee na kumuuliza kuhusu malalamiko hayo ya Bonge la Nyau.
“Ananijua na nadhani anayo namba yangu,” amesema Vanessa.
“Hatuna ugomvi na angekuwa ana nia angenicheki. Japo mpaka sasa sijui anachokiongelea and that’s because aliyemtuma simfahamu vizuri. Namfahamu zaidi yeye,” ameongeza.
Hii si mara ya kwanza msanii kudai kutoshwa na Vanessa kwenye collabo. Timbulo aliwahi pia kulalamika kupigwa mikausho.
0 comments :
Post a Comment