News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 7 January 2017

UNAKUMBUKA HII IVORYCOST WALIVYOFUNGWA UWANJANI WAKAJIKUTA WANAPELEKWA SELO?

Image may contain: 1 person, hat

Michuano Ya AFCON 2017 itaanza nchini Gabon Januari 14. Ni burudani nyingine kwetu wapenda soka. Jirani zetu Uganda wanashiriki. Vivyo hivyo DRC Congo.

Moja ya miamba ya michuano hiyo ni Ivory Coast. Ni taifa linalotarajiwa kufanya vizuri.
Hata hivyo, Ivory Coast wametoka mbali katika kufikia hatua hii ya ubora. Huenda si wengi wenye kukumbuka. Ni kwamba, mwaka 2000, Ivory Coast ilitolewa mapema kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika. Na Rais wa nchi wakati huo, Jenerali Robert Guei , alikasirika sana kiasi cha kuamuru, kuwa pindi watakapotua Ivory Coast, kikosi kizima cha timu ya taifa kipelekwe ndani ya kambi ya jeshi kikafundishwe uzalendo. Kwamba Rais aliamini kushindwa kwa Ivory Coast ni matokeo ya kukosa mioyo ya uzalendo.
Na kweli ikatokea, kikosi kizima kiliishia kuwekwa kambini jeshini na kufanyishwa kazi ngumu ikiwamo kuimba nyimbo za uzalendo.
Hata hivyo, mchezo wa soka nao ulikuwa na  Rais wake, aliiitwa Sepp Blatter. Rais wa soka alipopata taarifa kuwa wachezaji wake wamefungiwa kambini, basi, Sepp Blatter akatoa tamko kali dhidi ya Jenerali, rais wa nchi, kuwa kitendo chake ilikuwa ni kuingilia mambo ya ' Utawala wa soka wa Sepp Blatter'.
Wachezaji wale wakaachiwa huru, ni baada ya siku tatu ndani ya kambi ya jeshi.
Na Jenerali Robert Guei mwenyewe siku zake za kukaa madarakani zikawa zinahesabika, ilipofika mwezi Oktoba mwaka 2000, naye akapinduliwa!
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment