News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday, 20 December 2016

Mpambano wa Pogba vs kaka yake waleta mafuriko ya manunuzi ya ticket mpaka zimezuiwa kuuzwa!!



St Etienne wamepiga stop kuuza ticket za mechi
ya Europa dhidi ya Manchester United masaa
machache baada ya kuanza kuziuza. Kufunga
huko kumetokana watu wengi kujazana
wakitaka kununua hizo ticket licha ya
mabadiriko makubwa kwenye bei kama
ilivyozoeleka.


Watu wengi wanataka kuona mechi hiyo
ambayo itaifanya pia St Etienne ionekane sana
duniani kutokana na kucheza na Manchester
United. Mashabiki wanataka pia kuona club
yao ikicheza dhidi ya mastaa wa EPL.
Kitu kingine kizuri ni pale wanapotaka
kumuona mtu na kaka yake wakicheza dhidi ya
timu tofauti. Paul Pogba atakuwa anakabwa na
kaka yake Florentin Pogba ambae anacheza St
Etienne.


Kutokana na kuzuia kuuzwa kwa ticket hizo, St
Etienne wamewapa nafasi ya upendeleo
mashabiki wenye ticket za msimu mzima
(Season ticket holders) nafasi ya kununua
ticket hadi nne kila mtu hadi ikifika Dec 23 na
wengine wafuatie.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment