EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Desemba 10
Watford 3 Everton 2
Arsenal 3 Stoke City 1
Burnley 3 Bournemouth 2
Hull City 3 Crystal Palace 3
Swansea City 3 Sunderland 0
2030 Leicester City v Manchester City
++++++++++++++++++++++
Mechi 4 za EPL, LIGI KUU ENGLAND zimechezwa kuanzia Saa 12 Jioni hii Leo na ifuatayo ni Taarifa fupi ya Mechi hizo.
ARSENAL 3 STOKE CITY 1
Huko Emirates, Wenyeji Arsenal walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Stoke Bao 3-1 na kuishika Chelsea kileleni mwa EPL wote wakiwa na Pointi 34 lakini Arsenal wako juu kwa Ubora wa Magoli.
Arsenal walilazimika kumuingiza Hector Bellerin Dakika ya 25 kumbadili Mustafi alieumia.
Stoke walifunga Bao lao kwa Penati ya Kepteni wao Charlie Adam iliyotolewa na Refa Lee Mason kufuatia Granit Xhaka kumpiga Kipepsi Joe Allen bila kupewa Kadi yeyote mbali ya kutolewa hiyo Penati.
Theo Walcott aliirudisha Arsenal kwenye Gemu kufuatia Bao lake safi la Dakika ya 42 alipounganisha Pasi ya Bellerin.
Hadi Haftaimu Arsenal 1 Stoke 1.
Kipindi cha Pili Arsenal walifunga Bao 2 nyingine kwenye Dakika za 49 na 75 Wafungaji wakiwa Mesut Ozil na Iwobi.
VIKOSI:
Arsenal: Cech, Gabriel, Mustafi [BellerĂn 25'], Koscielny, Monreal, Xhaka, Coquelin, Walcott, Ozil, Oxlade-Chamberlain, Sanchez.
Akiba: Gibbs, Lucas Perez, Giroud, Ospina, Iwobi, Bellerin, Elneny.
Stoke City: Grant, Johnson, Muniesa, Martins Indi, Pieters, Allen, Imbula, Shaqiri, Adam, Arnautovic, Diouf.
Akiba: Whelan, Bony, Given, Crouch, Krkic, Sobhi, Ngoy.
REFA: Lee Mason
BURNLEY 3 BOURNEMOUTH 2
Wakicheza kwao Uwanjani Turf Moor, Burnley wameifunga Bournemouth Bao 3-2.
Bao 2 ndani ya Dakika 3, Dakika za 13 na 16, walizofunga Jeff Hendrick na Stephen Ward, ziliwapa Burnley uongozi wa 2-0 hadi Mapumziko.
Bournemouth walipata Bao Dakika ya 47, Dakika za Majeruhi Kipindi cha Kwanza, alilofunga Benik Afobe na Gemu kwenda Haftaimu ikiwa 2-1.
Kipindi cha Pili Burnley walifunga Bao lao la 3 Dakika ya 75 kupitia Boyd na Bournemouth kufunga Bao lao la pilli Dakika ya 91 Mfungaji akiwa Daniels.
VIKOSI:
Burnley: Heaton, Lowton, Mee, Keane, Ward, Arfield, Hendrick, Marney, Defour, Boyd, Vokes.
Akiba: Flanagan, Gray, Barnes, Kightly, Bamford, Robinson, Tarkowski.
AFC Bournemouth: Boruc, Francis, Steve Cook, Ake, Daniels, Adam Smith, Arter, Gosling, Fraser, Afobe, Callum Wilson.
Akiba: Pugh, Brad Smith, King, Federici, Mings, Wilshere, Ibe.
REFA: Martin Atkinson
HULL CITY 3 CRYSTAL PALACE 3
Ndani ya Kingston Communications Stadium, Wenyeji Hull City, chini ya Meneja Mike Phelan aliekuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Manchester United, wametoka 3-3 na Crystal Palace.
Hull walipata Bao kwa Penati ya Robert Snodgrass katika Dakika ya 27 baada ya mwenyewe kuangushwa na Scott Dann.
Palace walijibu kwa Bao 2 za Dakika za 52 na 70 walizofunga Christian Benteke na Wilfried Zaha na kuongoza 2-1.
Hull walisawazisha Dakika ya 72 kwa Bao la Diamande na kwenda mbele 3-2 katika Dakika ya 78 Mfungaji akiwa Jack Livermore.
Lakini Palace waliambua Sare katika Dakika ya 89 kwa Bao la Frazier Campbell.
VIKOSI:
Hull City: Marshall, Davies, Dawson, Maguire, Elmohamady, Livermore, Huddlestone, Clucas, Robertson, Snodgrass, Diomande.
Akiba: Meyler, Maloney, Jakupovic, Weir, Henriksen, Bowen, Mason.
Crystal Palace: Hennessey, Ward, Dann, Delaney, Kelly, McArthur, Ledley, Zaha, Puncheon, Townsend, Benteke.
Akiba: Speroni, Flamini, Cabaye, Campbell, Lee, Fryers, Phillips.
REFA: Mike Jones
SWANSEA CITY 3 SUNDERLAND 0
Liberty Stadium Leo ilishuhudia Wenyeji Swansea City wakiwatandika Sunderland 3-0 na kujichomoa toka mkiani.
Bao zao zilifungwa na Sigurdsson, kwa Penati ya Dakika ya 51, na Bao 2 za Fernando Llorente za Dakika ya 54 na 80.
VIKOSI:
Swansea City: Fabianski, Rangel, Mawson, Amat, Taylor, Fulton, Britton, Barrow, Sigurdsson, Routledge, Llorente.
Akiba: van der Hoorn, Fer, Nordfeldt, Montero, Cork, Naughton, McBurnie.
Sunderland: Pickford, Jones, Kone, Djilobodji, Van Aanholt, Pienaar, Ndong, Denayer, Larsson, Defoe, Anichebe.
Akiba: Mannone, Borini, Khazri, O’Shea, Manquillo, Kirchhoff, Januzaj.
REFA: Craig Pawson
EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumapili Desemba 11
1500 Chelsea v West Bromwich Albion
1715 Manchester United v Tottenham Hotspur
1715 Southampton v Middlesbrough
1930 Liverpool v West Ham United
Jumanne Desemba 13
2245 Bournemouth v Leicester City
2245 Everton v Arsenal
Jumatano Desemba 14
2245 Middlesbrough v Liverpool
2245 Sunderland v Chelsea
2240 West Ham United v Burnley
2300 Crystal Palace v Manchester United
2300 Manchester City v Watford
2300 Stoke City v Southampton
2300 Tottenham Hotspur v Hull City
2300 West Bromwich Albion v Swansea City
Jumamosi Desemba 17
1530 Crystal Palace v Chelsea
1800 Middlesbrough v Swansea City
1800 Stoke City v Leicester City
1800 Sunderland v Watford
1800 West Ham United v Hull City
2030 West Bromwich Albion v Manchester United
Jumapili Desemba 18
1630 Bournemouth v Southampton
1900 Manchester City v Arsenal
1900 Tottenham Hotspur v Burnley
Jumatatu Desemba 19
2300 Everton v Liverpool
KWA HABARI ZAIDI NA PICHA NYINGI ZA MICHEZO HIO BONYEZA HAPA!!




0 comments :
Post a Comment