News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 5 November 2016

MOURINHO ASEMA TIMU YAKE YA MAN UNITED INACHEZA KAMA INACHEZA MECHI ZA KIRAFIKI


Meneja wa Manchester United Jose
Mourinho amesema wachezaji wa
Manchester United walichukulia mechi
dhidi ya Fenerbahce katika Europa League
kana kwamba ilikuwa mechi ya kirafiki ya
kujiandaa kwa msimu.
Red Devils walishuka hadi nambari tatu kwenye
Kundi A ligi hiyo ndogo ya Ulaya baada ya
kulazwa 2-1 na klabu hiyo ya Uturuki mjini
Istanbul.
Manchester United sasa wameshinda mechi
mbili pekee kati ya saba walizocheza
mashindano yote karibuni.
"Timu inayofunga baada ya dakika mbili pekee
ni timu ambayo haiko tayari, haijajiandaa
kiakili, haina mwelekeo na haina umakinifu,"
amesema Mourinho.
United wamefunga mabao mawili pekee mechi
zao nne walizocheza karibuni zaidi.
Aidha, walifungwa baada ya sekunde 30 pekee
na Chelsea na sekunde 65 na Fenerbahce.
Mshambuliaji Moussa Sow alifunga kwa
kombora la kushangaza la kupitishia mpira juu
ya kichwa, naye Jeremain Lens akaongeza
jingine kupitia frikiki kabla ya Wayne Rooney
kufunga bao la kufutia machozi mechi
ikikaribia kumalizika.
Bado lake hilo la dakika ya 89 limemuwezesha
kufikia magoli 38 Ulaya na kufikia rekodi ya
Ruud van Nistelrooy.
Hata hivyo, amefunga mabao mawili pekee
katika mechi 17 alizocheza msimu wote.
Mourinho amesema: "Matatizo yetu yalianza na
mtazamo wetu wa kiulimwengu. Walikuwa
wanacheza fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya, tulikuwa tunacheza mechi ya kirafiki ya
majira ya joto. Huo ndio uhalisia wa jinsi
mechi ilianza.
"Walistahili kushinda, soka haihusu tu ubora,
kuna kutia juhudi pia, kujitolea, kujituma na
kujitolea kabisa. Lazima ucheze dakika zote 90
kwa hamu na umakinifu.
"Katika mazingira kama haya, kuwapa nafuu
wapinzani wako (kwa kufungwa mapema), hapo
ndipo wanataka kuwa. Kisha, tulituliza kasi ya
uchezaji na kuanza kumshinikiza refa, kuigiza
kwamba tumechezewa vibaya na hayo ndiyo
makosa yetu."
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea hata hivyo
alikiri kuwa "moja ya mambo mazuri leo ni
kwamba Rooney hatimaye amefunga bao."
Kati ya wachezaji walionunuliwa na Mourinho
majira ya joto - Paul Pogba, Zlatan
Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly
- ni Mfaransa Pogba pekee aliyeanza mechi.
Hata hivyo, aliondoka kabla ya kipindi cha
kwanza kumalizika akionekana kuumia.
Ibrahimovic aliiingia nafasi yake.
Mkhitaryan naye alichezeshwa mara ya kwanza
tangu 10 Septemba. Aliingia dakika ya 61
nafasi ya Marcus Rashford. Beki wao Bailly
anatarajiwa kukaa nje miezi miwili kutokana na
jeraha la goti.
Haijabainika jeraha la Pogba ni mbaya kiasi
gani na iwapo ataweza kucheza dhidi ya
Swansea Ligi ya Premia Jumapili.
Majeruhi United
Pogba, aliyetoka Juventus, amejiunga na
orodha ya majeruhi wengi United amba
wanajumuisha mabeki:
Eric Bailly (kano za goti) - hatacheza hadi
Desemba
Antonio Valencia (mkono) - haijulikani
atarejea lini
Chris Smalling (mguu) - haijulikani atarejea
lini
Magazeti Uingereza yalivyoandika baada ya
United kuchapwa:
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment