WINGA
Gareth Bale ataikosa mechi ya mahasimu wa Hispania, El Clasico Desemba 3
baada ya Real Madrid kuthibirisha ameumia kifundo cha mguu wa kulia.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 pia yuko hatarini kuukosa mchezo mwingine
wa Madrid na Borussia Dortmund kuwania usukani wa kundi katika Ligi ya
Mabingwa.
Na
wakati wanatoa taarifa hiyo leo, dawati la tiba la klabu lilikuwa
halijakamilisha vipimo ili kujua kama atahitaji upasuaji, lakini
limehakikisha atacheza Klabu Bingwa ya Dunia mwezi ujao.

Real
Madrid wataanzia katika Nusu Fainali ya michuano hiyo nchini Japan
Desemba 15 na wangependa mchezaji wao huyo wa pili kulipwa vizuri baada
ya Cristiano Ronalo awepo.
0 comments :
Post a Comment